Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.
MSHINDI wa Droo ya Maokoto Ndani ya Kizibo, Nazir Chonya amejishindia zawadi ya pesa kiasi cha Shilingi 500,000 baada ya kushinda katika droo hiyo.
Chonya amekabidhiwa kiasi hicho cha pesa leo, Mtaa wa Kibaoni Mkoani Iringa na Afisa Masoko Kampuni ya Vinywaji vya Serengeti Mkoani humo, Venance Kavishe, ambapo alimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa.
Kufuatia promosheni ya “Maokoto Ndani ya Kizibo”, iliyozinduliwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na kampuni hiyo, inayo mtaka mteja wa vinywaji vya kampuni hiyo, kuingiza tarakimu zilizo ndani ya kizibo kupitia simu yake.
Ili aweze kujipatia bahati ya kushinda, ambapo kati ya vinywaji hivyo ni pamoja na Serengeti Lite, Serengeti Lager, Pulsner Lager, Guineas Smooth, na Smirnoff.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi