January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chongolo:Viongozi acheni kulalamika,fanyenikazi

Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Daniel Chongolo amewakemea baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwa kuendeleza malalamiko badala ya kufanya kazi kwa kutimiza majukumu yao.

Mbali na kuwakemea Viongozi hao amewatangazia kihama viongozi hao ambao wanatumia muda mwingi kulalamika na kueleza kuwa kulalamika kwao kunaonesha wazi kuwa hawatoshi na kama hawawezi kufanya kazi wakae pembeni.

Chongolo amesema hayo jijini hapa leo,Januari 24,2023,wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wajumbe wa Sekretarieti mpya ya chama hicho ambao ni Daniel Chongolo-Katibu Mkuu wa CCM,Anamiringi Macha-Naibu Katibu Mkuu CCM Bara,Mohamed Said Mohamed-Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Sophia Mjema-Katibu wa Nec Idara ya Itikadi na uenezi,Dkt.Frank Hawassi-Katibu wa Nec Idara ya Uchumi na Fedha ,Mbarouk Nassor Mbarouk-Katibu wa Nec,Idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa (SUKI) na Issa Haji Ussi(Gavu)-Katibu wa Nec Idara ya oganaizesheni.

“Changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ndani ya chama chetu ni kuwepo kwa baadhi ya watumishi ndani ya serikali kuendelea kulalamika,unamkuta waziri aliyepewa dhamana ya kutimiza wajibu wake,Mkuu wa Mkoa na mkuu wa Wilaya badala ya kutimiza wajibu wao bado wao wanaendekekeza kulalamika.

“Hii ni aibu mfano unawakuta watumishi wa serikali wanaenda kwenye vyomba vya habari wanawalalamikia watendaji waliopo chini yao kuwa hawasaidie kufanya kazi kwa kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa hautoshi ni sawa na katibu mkuu kuwalalamikia waliopo chini yake kuwa hawasaidii kazi je unawezaje kulalamika wakati unatakiwa kutumia mamlaka uliyo nayo”amesema Chongolo.

Pamoja na mambo na mambo mengine Chongolo alisema kuwa Sekretarieti imeaminiwa zaidi kwa ajili ya kuhakikisha inafanya kazi kwa nia ya kuhakikisha inatatua matatizo ya watanzania na kujibu hoja.

“Chama chocote cha siasa kina kazi ndogo tu kutafuta na kushika dola sasa kazi yetu ni kutafuta na kushika dola sasa tunakazi ya kusimamaia dola tuliyopewa na dhamana ya kuishika na wananchi ili ifikapo 2025 tusiende kuulizwa na wananchi.

“Ndugu zangu 2019 chama kilipewa dhamani ya kushika nafasi za serikali za mitaa wajibu huo unatakiwa kusimamaia ili yuendeleee kuaminiwa zaidi na zaidi ndugu zangu wajibu huo si wakulaa kilegelege,kulala wala kuzembea .

“Changamoto nyingine tulitonayo kwa baadhi yetu ni baadhi ya watumishi waliopewa majukumu lakini lakini hawajui majukumu ya nafasi tulizopewa ,mkuu w mkoa badala ya kutimiza wajibu wake anakaa analalamika hatupo kwenye wajibu wa kusikiliza malalamiko yuko kwenye ajibu wa kutenda kama waxiri umepewa dhamana ya kutjmikia unashindwa kutumikia unachelewesha kutimiza malengo huo ndio wajibu tunaonenda kuufanya na tutaufnaya kwelimwkweli.

“Wananchi wanataka miungdo mbinu wananchi wanataka dawa za mifugo wannchi wanataka huduma sio maneneo,kama ni wachimbaji wadogo na wakubwa watendedewe haki sawasawa kama ni wakandarasi wa ndani na nje watendewe sawasawa wasipotendewa sawasawa watatuonyoshea kidole tukiruhusu wananchi watunyooshee vidole tutakua hatutendi sawasawa”ameeleza Chongolo.

“Mimi ni chongolo ila nikiwa hapa mimi ni Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi hivyo sitaki kuona viongozi watakaosababisha maswali mengi kwa watanzania yasiyokuwa na majibu ntunataka vitendo siyo maneneo,”amesema.

Katika hatua nyingine Chongolo amesema kuwa Wiki hii wanaanza ziara mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi kuanzia ngazi ya shina huku akiwataka watendaji wa juu wakihakikisha wanatoa ushirikiano na watumishi wa ngazi ya chini.

Aidha Chongolo amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kuchekeana na kufimbiana macho katika mambo ya msingi ambayo yanagusa maisha ya watu.

“Katika kipindi hiki msitegemee kuwa tutamfumbia macho mtu Moja ya changamoto tuliyonayo njnkhchekeana kwenye mambo ya kwelj kuoneana aibu kwa mambo tunayoyafanya,”amesema.