Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Tunduma
Wananchi wa Mkoa wa Songwe wanatarajia kupata maji safi na salama baada ya kusainiwa mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji wa Tunduma-Vwawa utakao gharimu kiasi cha bilioni 119.95.
Mradi huo unatarajiwa kuwahudumia wakazi 219,309 wa miji ya Tunduma, Vwawa, na Mlowo, hatua inayoakisi dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha huduma zkijamii.
Mradi wa Maji wa Tunduma-Vwawa unatarajiwa kuanza mara moja na kukamilika ndani ya miezi 18, hatua inayotarajiwa kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa Songwe.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo,katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi huo iliofanyika Machi 20, 2025, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Ambapo Mkataba huo ulisainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, kwa niaba ya Serikali, na Meneja Mradi wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Ning Yunfeng.
Chongolo amesisitiza kuwa Serikali ya Mkoa wa Songwe itahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vya juu ili wananchi wapate huduma bora.

Sanjari na hayo Chongolo, amesema Mkoa wa Songwe umepokea zaidi ya tilioni moja kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
More Stories
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya
Kenya,Uganda zaanzisha mradi wa uendelezaji rasilimali za maji Angololo