January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chongolo awacharukia makatibu wa UWT

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Taifa Daniel Chongolo
amelitaka Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho Taifa kujenga msingi wa kujitegemea na kuimarisha uchumi wa Jumuiya hiyo  ili waepukane na kuwa ombaomba.

Chongolo ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa lililofanyika katika ukumbi wa White House jijini Dodoma huku akiitaka Jumuiya hiyo  kutengeza mfumo imara wa kuwa na wanajumuiya wanaopjitambua ikiwemo wanachama ili waweze kuwa na Jumuiya zitakazoleta maendeleo katrika jamii.
Alisema UWT wanapaswa kuwa wabunifu katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo
itainua uchumi wao.

Vile vile amewataka kuhakikisha pamoja na mambo mengine wanaongeza wanachama kusimamia uhai wa chama katika ulipaji ada wa wanachama.

“Niwaombe acheni kulalamika fanyeni kazi,kuna viongozi hapa hapa wakiwemo makatibu hawafanyi kazi,unakuta mtu mkoa wake ukusanyaji wa ada ni asilimia moja au sifuri hivi mtu kama huyu unaweza kumfikiria kweli,

“Na wapo makatibu wa wilaya ambao wamekaa katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka hata mine l;akini yupo katibu wa wilaya ambaye amekaa mwaka mmoja tu katika nafasi hiyo na akapandishwa kuwa katibu wa mkoa ,hii ni kutokana na utendaji kazi wake na siyo vinginevyo.”amesema Chongolo

Amewataka watekeleze majukumu yao kama  Ilani ya CCM inavyosema ili kuwa na  Jumuiya Imara inayoleta maendeleo kwa watu.
Vile vile ameitaka Jumuiya hiyo kujenga mfumo imara ambao utawawezesha kuwa na
wanachama bora ambao wataunda Jumuiya bora yenye uhai.
Amesema wanatakiwa kuwa wanachama hai ambao wanajitambua kwa
kutekeleza majukumu yao ya kila siku ndani ya Jumuiya.
Amesema lengo lao ni kuona UWT inakuwa imara kila kukicha kwa sababu
ni umoja mkubwa unaotambulika kila mahali hapa nchini.
Hata hivyo amewapongeza viongozi wa Jumuiya hiyo wa wilaya na mikoa waliofanya
vizuri katika kuongeza idadi ya wanachama na ulipaji ada . Alisema wale waliofanya vizuri anachukua majina yao na kuyaweka kwenye
rekodi kwa ajili ya kufanyiwa kazi kama kuna kupandishwa nafasi.
Amesema kuna viongozi ndani yam waka mmoja wamepandishwa nyazifa zaidi
ya mara mbili au tatu kutokana na juhudi wanazofanya katia uongozi waliokabidhiwa.

Awali Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka alisema,Baraza hilo limetambua mikoa mitano iliyofanya vizuri katika usimamizi wa miradi iliyopo na kuanzisha mirdi mipya katika mikoa ytao.

Amesema,lengoi la kufanya hivyo ni kuwatia hamasa viongozi wote katika mikoa ili wafanye kazi kwa wledi na ujasiri na hatimaye kuongeza mapato ya Jumuiya hiyo.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Kuisni Unguja,Mjini Unguja,Kaskazini Pemba,Geita na Tanga.

Aidha amesema Barza hilo limempongeza Rai Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongeza nchi huku akizingatia maslahi mapana kwa wanawake.

“Katika hotuba zake Rais Samia anajipanga na kufnya utafiti ,ni hotuba zenye upendo,lakini pia hivi karibuni tumeona akizindua kamati Maalum ya Kijinsia iliyolenga katika kukuza masuala ya kiuchumi kwa akina mama,Baraza linampongeza sana.”amesema Kabaka