Na Zena Mohamed, Timesmajira o Online, Kongwa.
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi na Kampuni ya Rachi za Taifa – NARCO zimeagizwa kuwawezesha zaidi wafugaji wadogo ili watoke katika kilimo cha kawaida na wafikie daraja la kilimo cha Biashara.
Agizo hilo limetolewa jijini hapa leo Juni 17,2023 na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Daniel Chongolo alipotembelea NARCO Ranchi ya Kongwa,Mkaoni Dodoma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika majimbo yote ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza katika Ranchi hiyo Chongolo amesema kuna wafugaji ambao wana mifugo mingi lakini haiwanufaishi kutokana na kukosa elimu ya ufugaji kibiashara pamoja na kutumia mazao ya ng’ombe kama ngozi na pembe katika matumizi yasiyo na tija kwao.
Amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi eneo la mifugo bado wako nyuma kuwawezesha wafugaji wa kawaida kufuga kibiashara bado wanafuga kienyeji sana hivyo wanatakiwa kuwawezesha ili kufikia uzalishaji wa nyama wenye tija kwa biashara.
Aidha ameagiza kupelekwa mbegu maeneo ya malisho ya wakulima wa kawaida ili kulima mazao ya ng’ombe yatakayosaidia katika malisho,hasa katika kipindi cha kiangazi ambacho kuna changamoto ya malisho.
“Mimi niseme nimebahatika kukaa kule Longido kwa wafugaji wanafuga kimasikini sana lakini ukiwaona mtu ana ng’ombe 1000 lakini analalia ngozi mtu ana ng’ombe 500 lakini hawezi kupeleka mtoto shule kwasababu hajui kama ile ni fedha,”.
Hivyo amesema sasa ni wakati muafaka si tu kuangalia uzalishaji wenu nendeni mkaangalie na kufikiri sasa kupeleka elimu na kupeleka mbegu kwenye maeneo ya malisho ya wananchi ambayo yametengwa kwajili ya malisho.
“Wakati wa masika wakamwaga ile mbegu wakati wa kiangazi wafugaji wanauhakika wa malisho na unenepeshaji unaanza hukohuko kuja huku kwa majani ambayo ni majani mazuri ambayo ndiyo yaliayotengenezwa kwajili ya mifugo wakija huku hupati shida ya matatizo ya nyama ambayo mnaenda kuitengeneza na kuizalisha hayo ndiyo ya msingi,”amesema na kuongeza kuwa
“Wakati mnafanya hiyo ya kwenu na mimi nitaiwekea msukumo kuhakikisha hilo linatokea lakini bahati mbaya nikienda nikasoma nikajiridhisha kuweka msukumo wa nyinyi kupata hiyo fedha ujue hiyo fedha tutaifuatilia hadi tone la mwisho ili mturidhishe kwa kile tulichopinga katika kuzalisha kwa tija,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NARCO Peter Msofe ameiomba serikali kuwawezesha katika miradi miwili yenye thamani ya bilioni 84 yenye lengo la kutoa elimu kwa wanawake na vijana kuhusu ufugaji pamoja na mradi wa unenepeshaji ng’ombe.
Ranchi hiyo ya Kongwa ina hekta 38,000 ambapo ndani yake kuna mifugo 30000,huku hekta 18,000 wakipewa wawekezaji wakiwemo wananchi.
More Stories
Mwinyi: Kuna ongezeko la wawekezaji Zanzibar
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi