December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Historia imeandikwa Tanzania, baada ya Mkanda mwingine kubakia katika Ardhi ya Tanzania ambapo Bondia Said Mohamed maarufu kama Said Chino kuwa bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship kwa kumchapa mpinzani wake raia wa Afrika Kusini Lusanda Komanisa kwa pointi.

Said Chino ameshinda pambani hilo kwa point kutoka kwa majaji wote watatu

Kwa ushindi huo Said Mohamed amezwadia #KnockoutyaMama ya Shilingi milioni tano kama zawadi , ambapo katibu mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema kuwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuisapoti sekta yote ya michezo na kwasasa mapambano yote ya kimataifa yatakayohusisha mabondia wa Kitanzania basi Mh. Rais Samia atakuwa motisha kwa mabondia hao

KnockoutyaMAMA