November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Charamila mgeni rasmi mbio za TCAA

Na Irene Clemence, TimesMajira Online

KATIKA kuadhimisha miaka 20 ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA) imeandaa mbio za km 5 mpaka 10 zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 katika Viwanja vya Mlimani City huku Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Charamila akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa maandalizi ya Maadhimisho hayo Mellenia Kasese ameyabainisha hayo Jijini Dar es salaam mapema Leo Octoba 26 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini kuhusiana na mbio hizo amesema mbio hizo ni sehemu ya muendelezo wa matukio ya kusherehekea miaka 20 ya taasisi hiyo ambayo tangu ilipoanzishwa.

Amesema lengo mbio hizo ni kutunisha mfuko wa upandaji miti katika katika jamii hasa katika maeneo ambayo ni kame .

“Mbio hizo zitakuwa za km tano na kumi,maandalizi yameshakamilika vifaa vyote vimeshafika na mpaka sasa tunavyoongea tiketi zote 400 ambazo zilitengwa kuuza kwa ajili ua washiriki zimeshaisha siku tatu nyuma,”amesema Kasese.

Naye katibu wa Chama Cha Riadhaa Mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela ambao ndiyo wasimamizi wa mbio hizo amesema tangu awali wamekuwa wakishirikiana na TCAA katika maandalizi y mbio hizo wamekuwa walishirikiana vyema katika maandalizi kutokana na Chama hicho ndio limekuwa kikiusika katika mbio zote.

“Tumejiridhsiha na tumrhakikisha njia zitakazotumika kwanza zimepimwa na salama,tunasubiri Jumapili kwa ajili yakuhitimisha tukio lenyewe,”amesema Mwela.

Aidha ametoa wito kwa wadau wengine wanaofanya mbio za hisani kushirikiana na Chama hicho Ili kuweza kuepukana na chagamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.

“Kumekuwa na changamoto kwa watu wengine kutohusisha chama cha riadha wanapoandaa mbio ni hatari sana ukipata jambo utakuwa hauna pakupeleka kama hivi wamefanya jambo la kuhimu na kuweza kujua nini chakufanya,”amesema Mwela.