December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chande azindua misheni ya uangalizi uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC (SEOM) katika Uchaguzi Mkuu wa Mauritius Jaji(Mstaafu) Mohammed Chande Othman, amezinduamisheni hiyo jijini Port-Louis, Mauritius, kwa niaba yaMwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Uzinduzi huo uliofanyikia kwenye Kituo cha Sanaa cha Caudan, pia umewaaga waangalizi wa uchaguzi 35 ambao wameondoka kwenda maeneo tofauti kwa ajili ya kazi hiyo.

Katika hotuba yake, Chande amebainisha kuwa dhumuni kuu la misheni hiyo ni kufanya tathmini ya mwenendo wa uchaguzi nchini Mauritius kwa kuzingatia katiba na kanuni za uchaguzi za nchi hiyo, pamoja na misingi iliyowekwa katika Kanuni na Miongozo ya SADC inayosimamia Uchaguzi wa Kidemokrasia.

“Dhamira yetu siyo tu kuangalia uchaguzi, bali ni kuchangia kwa njia ya kujenga, huku tukifanya tathmini ya kina kama uchaguzi unazingatia viwango vya kidemokrasia,” amesema Chande.

Akizungumza mbele ya wadau mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo ikiwemo Jumuiya ya Wanadiplomasia,Chande alitambua kazi kubwainayofanywa na SADC katika kusimamia chaguzi kwenyeukanda wa Kusini mwa Bara la Afrika ambapo alielezakuwa uchaguzi wa Mauritius ni sehemu ya mfululizo wachaguzi kwenye nchi wanachama saba wa SADC wenyetakribani raia milioni 130, taswira anayoakisi dhamira ya umuiya ya kuimarisha mabadiliko ya kidemokrasia.

SEOM, ambayo ilianza kazi zake za maandalizi yausimamizi wa uchaguzi nchini humo mnamo tarehe 28 Oktoba, inajumuisha waangalizi 73, kutoka nchi nanewanachama wa SADC.

Timu yaa waangalizi 35 iliyobobeakwenye masuala ya uangalizi wa chaguzi itapelekwakwenye majimbo yote ya uchaguzi ambapo wataangaliamasuala mazima ya maandalizi kabla ya uchaguzi, taratibu za siku ya uchaguzi, na shughuli baada ya uchaguzi. Vigezo muhimu vya uangalizi ni pamoja na uhuru wa wananchi kujieleza, upatikanaji wa vituo vya kupigia kura, muda wa kufunguliwa na kufungwa kwa vituovya kupigia kura, elimu ya wapiga kura, na haki ya taasisi za uchaguzi.

Chande amesisitiza kuwa mambo haya ni muhimu katika kuhakikisha kuwa uchaguzi sio tu unafuata taratibu, bali pia unakidhi matarajio ya kidemokrasia ya wananchi wa Mauritius.

Akijibu maswali ya waandishi wa Habari, Chande alisifu wananchi wa Mauritius kwa kuwa na imani kubwa na vyombo vyao vya kuendesha uchaguzi.

Amesema kuwa ni nchi chache sana barani Afrika ambazozina idadi kubwa ya wapiga kura, lakini pia kufanikishakuwasajili kwa asilimia 98 kwenye daftari la wapiga kura.

Amesema hii ni hatua kubwa sana ya demokrasia nchinihumo, na inahamasisha wananchi wengine barani Afrika kufuata nyayo hizo na kutimiza haki ya kikatiba.

Hivyo amewasihi wadau wote, ikiwemo vyama vya siasa, asasi za kiraia, na vyombo vya habari, kuendeshashughuli zao kwa amani ili uchaguzi huo ufanyike katika mazingira ya amani. Aliwahimiza wananchi wa Mauritius kujitokeza kwa wingi kama walivyojiandikisha, kutumia haki zao za kikatiba na kutimiza demokrasia kwa kupigakura na kuheshimu matokeo ya uchaguzi, ambayo SEOM itayaangalia kwa ukaribu. Taarifa ya awali ya matokeo ya uangalizi wa SEOM itatolewa tarehe 12 Novemba 2024, siku mbili baada ya kupigwa kura tarehe 10 Novemba,2024.

Wajumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Mauritius ina wajumbe wapatao 73 kutoka nchi nane (8) za Wanachama wa SADC ambazo ni Jamhuri ya Botswana, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe, Ufalme wa Eswatini na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waangalizi hao wa uchaguziwalipitia mafunzo ya siku nne kuanzia tarehe 1 hadi 4 Novemba 2024, ili kupata ufahamu na muktadha wa uchaguzi nchini Mauritius. Waangalizi hao watapelekwa katika wilaya kumi za utawala za Mauritius, ambazo ni, Black River, Flacq, Grand Port, Moka, Pamplemousses, Plaines-Wilhems, Port-Louis, Rivière du Rempart, Savanne na Rodrigues.