January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chama kuiongoza Simba dhidi ya FC Platinum, Bocco ndani

KIUNGO Mzambia, Clatous Chama amepewa kitambaa cha unahodha kuiongoza timu ya Simba katika mchezo wake wa marudiano wa Ligi Mabingwa Afrika dhidi ya FC platinum ya Zimbabwe.

Simba ina kibarua kizito cha kuhakikisha inapata ushindi wa zaidi ya goli mbili utakaowahakikisha kutinga katika hatua ya makundi baada ya kupoteza kwa goli 1-0 katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa zimbabwe.

Katika mchezo huo pia, Nahodha John Bocco aliyekosa mchezo wa kwanza ameanzia benchi pamoja na mshambuliaji Meddie Kagere.