January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chama haendi popote

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema kiungo wao kutoka nchini Zambia Clatous Chama ambaye hivi karibuni alikuwa akihusishwa kumalizana na majirani zao Yanga kuwa hatokwenda popote kwani yatari wameshamuongeza mkataba ambao utamfanya asalie ndani ya klabu hiyo hadi msimu wa 2022.

Hivi karibuni kiungo huyo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari jambo lililokuwa likiwapa presha mashabiki wa klabu hiyo ambao walikuwa wakiamini kuwa mchezaji huyo anaondoka klabuni hapo.

Akitolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo walijadiliana katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika Juzi, Mo amesema kuwa, hata kabla ya kuanza kusikika kwa tetesi hizo tayari walikuwa wameshamalizana na mchezaji huyo na ndio maana alikuwa kimya.

Amesema, hawakutaka kuliweka jambo hilo sasa hivi lakini kutokana na minong’ono mingi
ambayo ilianza kuwavuruga wana Simba wameona jambo hilo haliwezi tena kusubiri na kuamua kulitokea ufafanuzi.

Sisi kama viongozi tunajua umuhimu wa Chama kwani ni mchezazaji ambaye ameshafahamu mazingira na falsa ya Simba hivyo hatuwezi kumuachia kirahisi kama watu wanavyodhani
hivyo hatuwezi kumuacha kirahisi wengine waje kumchukua.

“Chama ana mapenzi na Simba na sisi wanasimba, wapenzi na mashabiki tunamapenzi nae na ni mchezaji mzuri ambaye amekuwa MVP huku akizoa tuzo nyingi msimu uliopita na ndio maana tuliona anastahili kuendelea kusalia kwentu hivyo tumeshaini nae mkataba atabaki na Simba hadi msimu wa 2022,” amesema Dewji.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema kuwa, pia tetesi zinazoendelea juu ya mshambuliaji wao Meddie Kagere kutaka kuondoka hazina ukweli wowote kama zilivyokuwa taarifa za Chama.

Amesema, kikubwa ni kwa mashabiki wao kusubiri kuanzia kesho kwani wataanza rasmi kuweka kwenye mitandao yao ya kijamii ni mchezaji gani anaondoka, yupi anabaki na yupi watamsajili.

“Siku hizi kuna propadanda nyingi zinazoendelea lakini sisi ni klabu inayofanya kazi kwa weledi hivyo tusiende na mambo haya, tuache muda uongee na kuanzia kesho tutaanza rasmi kuweka wazi usajili wetu kuwa ni nani anaondoka na nani atabaki ndani ya kikosi chetu” amesema Mo.