Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za maendeleo kwa wanachalinze kiasi cha Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Akizungumza hayo jana wakati wakupokea vyumba vya madarasa yaliyojengwa na fedha hizo,amesema takribani vyumba vya madarasa 80 yakiwemo Madarasa ya Sekondari 66 na Shule ya Msingi Shikizi 14 kwa upande wa Elimu.
Ridhiwani amesema kazi inaendelea ya kujenga maendeleo ya watu huku akitoa shukrani za wana Chalinze kwa Rais Samia kwa kuendelea kujali maisha ya Watanzania anaowaongoza.
“Kazi yetu ni kuhakikisha Ndoto na Maono yake yanatimia,Chalinze tumekamilisha ujenzi wa madarasa na Januari 4,2022, ilikuwa siku nzuri sana kwa wananchi wa Chalinze baada ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kupokea vyumba vya madarasa 80 ,”amesema na kuongeza
“Milioni 80 imetumika kwa ajili ya Bweni la wanafunzi wenye uhitaji maalum shule ya msingi Chalinze huku,Milioni 90 Nyumba ya Mganga Tatu kwa Moja Hospitali ya Wilaya Chalinze inayojengwa Msoga kutoka kwenye fedha za Uviko.” Amesema Ridhiwan
Amesema kuwa, miradi mbali inaendelea kujengwa na mingine imekamilika kupitia fedha hizo za Maendeleo Bilioni 1.7 zilizotolewa na Rais Samia.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi