Na George Mwigulu,Timesmajiraonline,Mpanda.
CHAMA Cha Demokrasia na Maendedelo (CHADEMA), Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi kimempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kwa kazi nzuri hususani ya usimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024.
Katibu wa CHADEMA wilaya ya Mpanda, Richard Mponeja akizungumza Novemba 12, 2024 na Waandishi wa Habari amesema kwamba uwajibikaji wa mkurugenzi huyo si wa kutiliwa shaka na unaonesha kutenda haki kwa masirahi ya utawala bora na demokrasia nchini.
Akiwa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho ya mkoa wa Katavi,Mbali na kumpongeza Mkurugezi wa manispaa hiyo Sophia Kumbuli. Kiongozi huyo wa Chadema ametoa wito kwa watu wenye dhamana ya kusimamia uchaguzi kutokuwa chazo cha kubaka demokrasia wakati wa uchaguzi.
“Niwe muwazi, mkweli na si mchoyo wa wadhira nimpongeze na kumsifia kwa asilimia 60 mkurugenzi wetu wa manispaa ya Mpanda amekuwa msikivu kila tunapompatia changamoto amechukua hatua kwa wakati ikiwemo yeye mwenyewe kuondoka ofisini kwake na kufika eneo husika” Amesema Katibu huyo.
Amesisitiza kuwa ameweza kukutana na viongozi mbalimbali wa chama hicho cha upinzani nchini na kutoa ushirikiano mkubwa licha ya maeneo mengine kupata chagamoto kwa baadhi ya wasimamizi wenye kudanganywa kuwa Mtendaji wa mtaa au kijiji anaweza kufutwa kazi na kada yeyote wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) jambo ambalo si kweli.
Ameongeza “Wasiwe na hofu warudi wakapitie sheria za ajira ambazo ndizo zinazolinda haki za wafanyakazi ili waone kama mwenyekiti wa kata wa CCM au Katibu anaouwezo wa kumfuta kazi kama hatampitisha mgombea wa CCM ambaye hajakidhi vigezo vya kanuni za uchaguzi”.
Kiongozi huyo wa upinzani, Amebainisha kuwa kiongozi yeyote atakayechaguliwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa atafanya kazi na watendaji huku akifuata maelekezo kwa sera ya taifa ambapo kwa pamoja watakwenda kusimamia fedha na miradi ya serikali.
Katibu CHADEMA Jimbo la Mpanda mjini, Sospter Chotola amesema tangu zoezi la uchaguzi limeanza kufanyika kuna baadhi ya mambo yamekwenda sawia kwa Mkurugenzi kwa kazi nzuri jambo wasimamizi wasaidizi wamekuwa hawatendi haki.
Amesema “Baada ya uteuzi wa Novemba 8, 2024 wagombea wengi wa jimbo la Mpanda mjini waliteuliwa na wachache hawakuteuliwa kwa sababu zisizo na mashiko. Na baada ya kuwa teua ikapita siku moja tu nilipokea taarifa ya mapigamizi kwa kata nane kwa wakati mmoja”
Maria Kapesa, Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Makanyagio manispaa ya Mpanda amesema kuwa ndani ya chama hicho ni wanawake watano pekee waliojikeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Amesema nia na uthubutu kama mwanamke kuweza kugombea nafasi ya uongozi ni kutaka kuibadilisha jamii yake kuamini katika kuwachagua wanawake kuwa viongozi wengi zaidi.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato