
Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amehitimisha maandamano ya leo January 24,2024 katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini Dar es salaam ambapo amesema wametuma barua yenye mashtaka yao kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mbowe amesema “Kama ambavyo mlitangaziwa maandamano yetu yalikuwa yanafikia tamati Ofisi za Umoja wa Mataifa, tumeleta mashtaka yetu kwenda kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa New York, Mwakilishi amepokea barua yetu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa UN, barua hiyo tuliyompelekea ikishapokelewa rasmi na Katibu Mkuu wa UN tutaisambaza kwa Vyombo vyote vya Habari, nakala yake tutaitoa kwa Umma baada ya Katibu Mkuu kuipokea kule New York”
“Kwa ujumla wake barua imebeba yaleyale ya msingi ambayo tumekuwa tukiyasema kila siku ikiwemo Serikali ya CCM kutotaka kusikia maoni ya Wananchi katika njia bora ya kuboresha mifumo ya Uchaguzi, kupata Katiba mpya na kupanda kwa gharama za maisha ambazo zinawatesa Watu”
“Mnaona tumefanya maandamano makubwa na marefu bila hata sisimizi kuumizwa na hiyo ndio tabia ya CHADEMA, pale Polisi wanapoelewa hoja zetu tunakuwa hatuna ugomvi na yoyote, tutaendelea kuandamana katika utaratibu na Mikoa mbalimbali hadi wenzetu watuelewe tunamaanisha nini”




More Stories
Simbachawene:Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji Rasilimaliwatu umebaini upungufu wa watumishi 441,366
Wakazi Arusha watakiwa kuchangamkia fursa huduma jumuishi za kifedha
Wahitimu wa Mafunzo ya Scout Nkasi watakiwa kuwa mwangaza kwa vijana