Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua Uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema la kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake 18 wakati wa kusikiliza rufaa za Wabunge hao, kutokana na kubainika Kwa wajumbe 23 waliotoa hukumu hiyo kupitia Kamati Kuu ya Chama hicho, kuhusika katika kusikiliza rufaa zao na kuitolea uamuzi katika Baraza Kuu.
Mahakama Kuu imefuta maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA ya kubariki kufukuzwa uwanachama Wabunge 19 wa Viti Maalum kwa sababu baadhi wa wajumbe kushiriki katika Kamati Kuu pamoja na Baraza Kuu.
Akisoma Hukumu hiyo Jaji Cyprian Mkeha amesema uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu shauri lililowasilishwa na wanachama hao ya kupinga kuvuliwa uanachama kwa madai ya kuuapishwa kuwa Wabunge wa Viti maalum bila idhini ya Chama, jambo ambalo Chadema inadai ni kinyume na taratibu za Katiba ya Chama.
Kuhusu hoja ya waleta maombi kudai hawa kupewa kupewa muda wa siku 14 kujitetea, Mahakama imebainisha kuwa walipewa nafasi ya kusikiliza na hawakuitumia, na kwamba Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba yake walikua na Mamlaka ya kusikiliza shauri lao Kwa njia ya dharura, na taratibu zote ambazo walistahili kuzizingatia zilizingatiwa, ispokua uamuzi wa Baraza Kuu wa kusikiliza rufaa za Mdee na wenzake uliofanywa na baadhi ya wajumbe walioshiriki kutoa uamuzi ndani ya Kamati Kuu jambao ambalo si sahihi.
Wakili Dickson Matata Alifafanua uamuzi wa kuwafuta uanachama ni maamuzi halali, hivyo mahakama imetengua maamuzi rufaa ya baraza kuu kwa sababu wajumbe ambaye ni Mwenyekiti na katibu wa kamati kuu iliyohusika kuwafuta uanachama, walikuwepo tena katika kikao cha wajumbe wa baraza kuu kupariki maamuzi ya kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Wakili Matata alisema kuwepo kwa mwenyekiti na katibu kupelekea mahakama kufuta maamuzi ya baraza kuu kutokana na kuonesha viashiria vya kutokuwa na haki lakini ameacha maamuzi ya kamati kuu ya kuwafuta wabunge 19 uanachama wa CHADEMA.
Kesi hiyo inayohusu uhalali wa utaratibu uliotumika kuwavua Uanachama Wabunge 19, kuna hatua ya mahojiano kati ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Mawakili wa Wabunge hao akiwemo Halima Mdee
Halima Mdee na wenzake 18 walipinga uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu iliyowafuta uanachama Novemba 27, 2020 kwa tuhuma za kuapishwa kuwa Wabunge bila ridhaa ya Chama.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best