Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali (CEOs Forum Annual General Meeting) umefanyika katika Hifadhi ya Ngorongoro, ukilenga kuimarisha mchango wa taasisi hizo katika kukuza uchumi na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mkutano huo umewakutanisha watendaji wakuu kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujadili fursa za kiuchumi na kuimarisha ushirikiano katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa.
Akiongoza kikao hicho akiwa Mwenyekiti wa Muda, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),Ephraim Balozi Mafuru, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano, ubunifu na uwajibikaji katika kuimarisha utendaji wa taasisi za Serikali na kuleta matokeo yenye tija kwa wananchi.

Majadiliano pia yamejikita katika namna taasisi hizo zinavyoweza kutumia rasilimali, teknolojia na fursa zilizopo katika sekta mbalimbali kuongeza ufanisi, kuchochea uwekezaji na kukuza biashara. Ushirikiano huo unaweka msingi wa kuunganisha huduma za taasisi na mahitaji ya wazalishaji, wafanyabiashara na wawekezaji katika safari ya kufikia malengo ya Dira 2050.




More Stories
Tanzania,Uganda zapiga hatua kiwanda cha kusafisha mafuta
Aliyejifanya mtumishi TANESCO anaswa akiwaunganishia wateja umeme
Kamati ya Bunge:Hatutakaa kimya miradi ya Umwagiliaji