CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetoa salamu za pole kwa familia na Taifa kwa ujumla kufuatia kifo cha mmoja wa waaaisi na viongozi waandamizi nchini, Cleopa Msuya, kilichotokea leo Mei 7, 2025 saa 3 asubuhi katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam.
Akitoa pole hizo kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema ” kwa namna ya kipekee tunaungana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi hiki cha maombolezo ya siku saba zilizotangazwa rasmi leo kwanzia Mwi 7 hadi 13 kwa heshima ya maisha na mchango wake mkubwa kwa Taifa” amesema Nchimbi.

More Stories
Kikundi cha Mwanamke Shujaa chamchangia Fedha ya kuchukua Fomu Rais Samia
Magugu maji yatajwa changamoto ya uzalishaji umeme maporomoko Rusumo
Wataalam Maendeleo ya Jamii waaswa kutoruhusu tamaduni potofu