May 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yatoa maelekezo kwa Serikali

Penina Malundo na Joyce Kasiki,Dodoma

SEKRETARIETI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Daniel Chongolo imeanza kazi ya kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kuzitaka Wizara kuzingatia vipaumbele vyenye kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijni Dodoma,Chongolo amesema kazi ya Serikali ni kutekeleza ilani ya chama hicho ambacho kimepata ridhaa kutoka kwa wananchi ili kiweze kutimiza matarajio yao.

“Serikali inaongozwa na chama kilichoshika dola,hivyo chama chetu kinatoa maelekezo kwa Serikali ,kwa zile wizara ambazo bado jazijawasilisha bajeti zao,lazima bajeti hizo zilenge katika vipaumbele vinavyokwenda kutatua changamoto za kila siku katika jamii.

Kwa kuanzia Chongolo amesema chama hicho kimetoa maelekezo katika wizara tatu ambazo ni pamoja na

Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Nishati.

Amesema serikali inapaswa kuzingatia manung’uniko ya wananchi kwenye bajeti zake kwa kuanzia na mwaka huu wa Fedha wa 2021/2022.

“Leo hii tumewaita ili kuwaeleza tulikuwa tunafanya nini tangu tulipoteuliwa kuingia kwenye Sekretarieti,kwa kipindi kifupi tuliona tushughulikie maeneo muhimu yanayoleta manung’uniko kwa Wananchi ili Serikali iyazingatie kwenye Bajeti zao,”alisema na kuongeza

“Kuanzia, leo tutaangalia na kutoa msisitizo wa Chama kwenye Sekta kubwa tatu za Ardhi, Kilimo, na Nishati kwa kuhakikisha katika bajeti zao zinaangalia Changamoto za wananchi na kuzitatua,”alisema