January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yaonya walioanza kampeni za ubunge

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi ABAS MTEMVU ametoa onyo kwa Makada wa chama cha Mapinduzi na Madiwani walioanza kampeni za Ubunge kabla muda wake .

Mwenyekiti Abas Mtemvu aliyasema hayo kata ya chanika Jimbo la Ukonga wakati Naibu Meya wa Halmashauri ya la Dar Es Salaam Diwani wa Kata ya Chanika Ojambi Masaburi, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi na kukagua miradi ya Maendeleo .

“Kuna Mbunge amenieleza kuna Madiwani wanne wameanza fujo za kampeni za Ubunge kabla wakati natoa onyo Muda wake bado naomba muwaache wafanye kazi zao za Utekelezaji wa Ilani ya chama waweze kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia miradi ya Maendeleo ” alisema Mtemvu .

Mwenyekiti Mtemvu aliwataka Madiwani na Wabunge waliopo madarakani wafanye kazi na kutangaza utekekezaji wa Ilani ya Chama inayofanywa na pochi la mama zikiwemo Shule vituo vya afya na miradi ya Maendeleo .

Aliwataka watangaze kazi zote zinazofanyika na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt,Samia Suluhu Hassan .

Wakati huohuo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupanga safu mpya ndani ya chama pamoja na Daniel Chongolo na sektretalieti nzima ya chama hicho .

Akizungumzia standi ya Daladala ya Chanika Videte alisema itakapokamilika itakuwa standi Bora ya kisasa Jimbo la Ukonga.

Alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala kwa Ubunifu wake na ufanyaji kazi za kutatua kero na kujenga chama .

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu alisema mradi wa Dampo la Pugu Kinyanwezi zipo Bilioni 85 za kuboresha Dampo ametaka Halmashauri ya Jiji kufatilia pesa hizo tuweze kupata Dampo la kisasa .

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa alisema Maji ya DAWASA yalikuwa kero Jimbo la Ukonga kwa Sasa Mradi wa DAWASA Ruvu juu mradi umeshatandazwa mabomba mpaka Buyuni Maji safi na Salama yanaelekea Chanika .

Diwani wa Chanika Ojambi Masaburi, akiwasilisha Ilani ya Chama ya utekelezaji miradi ya Maendeleo alisema kata ya Chanika inajivunia sekta ya Elimu imetekeleza kwa asilimia 100 madarasa ya Elimu msingi na Elimu Sekondari ,Nishati ya Umeme kwa Sasa Chanika yote mijijini Vijijini WANANCHI wanajivunia umeme .

Aidha alisema kata ya Chanika ina Mitaa minane kazi kubwa ya Maendeleo Chanika inafanywa na madiwani wa Halmashauri katika kusukuma Maendeleo ya Kata hiyo .

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alisema ndani ya Wilaya ya Ilala ameshafanya ziara mbalimbali za kutatua kero na ziara za chama pamoja na Vikao na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutatua kero na kupanga mikakati mbalimbali.

Diwani wa Chanika Ojambi Masaburi (kushoto wa Pili)akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Abas Mtemvu January 14/2023 wengine Mwenyekiti wa CCM Wilaya Said Sidde na Mwenyekiti wa CCM Chanika Wiliam Mwila .
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Diwani wa chanika Ojambi Masaburi akizungumza katika mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama January 14/2023.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu akipokea kadi ya ACT WAZALENDO kutoka kwa mmoja wanachama wa chama hicho katika ukumbi wa Butiama chanika ambapo wanachama wa kutoka vyama vya upinzaji walijiunga CCM kata ya chanika .
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akizungumza na Wana CCM wa Chanika wakati Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Diwani wa Chanika Ojambi Masaburi alipowasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama .