Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kimanga George Mtasingwa, amesema CCM imejipanga kushika dola katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 kwa kushinda mitaa yote mitano na Uchaguzi mkuu mwaka 2025 kura zote kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti Mtasingwa alisema hayo kwenye ziara ya Chama cha Mapinduzi CCM Kimanga katika operesheni Bendera kwa wajumbe wa mashina na kugawa reja kwa wajumbe wa mashina 81 pamoja na Vitendea kazi kwa viongozi wa chama na Jumuiya .
“CCM Kimanga pamoja na Kamati yangu ya siasa tumejipanga kushika dola katika chaguzi zote za Serikali ya Mtaa na Uchaguzi mkuu mwaka 2025 wa Rais , wabunge ,Madiwani naomba viongozi wangu wa chama mliopewa madaraka kujenga chama na kutatua kero za wananchi muwe wamoja “alisema Mtasingwa.
Alisema dhumuni la mkutano huo ni utekelezaji wa sehemu ya ahadi ya Diwani wa kata Kimanga Pastory Kyombiya ambapo ametoa vitendea kazi bendera 81 ,reja za wajumbe wa mashina 81 na miongozo na kanuni za chama na Jumuiya.
Mwenyekiti George Mtasingwa aliwataka viongozi wa chama waliopewa madaraka kujenga umoja na mshikamano ikiwemo kudumisha amani na Upendo waache makundi na kuwa vipande ,vipande wapunguze maneno wafanye kazi ccm itashinda kwa kishindo
Alisema CCM Kimanga ipo imara mitaa yote mitano itashinda ili ipate wabunge wao ,madiwani na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Alisema chama cha Mapinduzi CCM kimewapa nyezo ngazi ya matawi kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi kwani viongozi wana jukumu kubwa.la kuwatunza wanachama na kuwalea ikiwemo kuboresha reja zao kwa wanachama .
Aidha alisema wakati wa kusajili watasajili wanachama wote ambao bado kusajiliwa katika mfumo wa kadi za kisasa Electronic.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba