Na Daud Magesa, Timesmajira Online Magu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeibomoa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Magu mkoani Mwanza baada ya aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kata ya Magu mjini, Titus Gabriel kujiunga na CCM.
Gabriel akiongozana na Said Kishiwa pia mwanachama wa CHADEMA wametangaza uamuzi huo wa kujiunga na CCM Februari 5,2024 katika maadhimisho ya miaka 47 yaliyofanyika kimkoa wilayani Magu.
Akizungumza na Timesmajira Online Gabriel amesema wamejiengua CHADEMA na kujiunga na CCM kwa sababu ya ubinafsi wa viongozi wa juu wa chama hicho lakini pia kazi nzuri zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Chama nilichokuwa nikikipigania hakikutaka kushuka chini na kujishusha kwa wananchi kufanya kazi na ubinafsi wa viongozi wa CHADEMA umesababisha nijiunge na CCM bila kushawishiwa na mtu,”amesema.
Gabriel amesema kiongozi sababu zilizomvuta kujiunga na CCM ni kazi anazozifanya Dk.Samia na namna anavyoshuka chini kusilikiza kero za wananchi na kutatua.
“Kumbukumbu ziko vizuri hakuna asiyeijua kazi niliyoifanya nikiwa Chadema mwaka 2015 hadi 2017 niliwapiga kwa kupata viti vingi serikali za mitaa,nawashukuru kwa kunipokea sasa niko tayari kuitumikia CCM,”.
Kwa upande wake Kishiwa amesema waliyokuwa wakiyapigania Rais Dk.Samia anaendelea kuyatatua na kuyafanyia kazi na hivyo anawashukuru wana CCM kwa kumpokea kundi na mjomba wake ushirikiano.
Akizungumza baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ amesema
” Nawapongeza wageni wetu waliojiunga nasi karibuni nyumbani, leo ninyi ni sawa na wana CCM wengine tuchape kazi.”
Mbali na wanachama hao wawili mwingine pia kutoka Chadema alijiunga na CCM katika Shina namba 21 Kata ya Bujora wakiwemo wengine wapya zaidi ya 16,”.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa