Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Chama Cha Mapinduzi CCM kimefunga Kampeni zake za kunadi sera zake kupitia chama hicho, na kuwakumbusha Wananchi kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa ifikapo siku ya jumatano,tarehe 29, 2025, kumchagua Rais, Mbunge na Diwani kupitia chama hicho.
Akizungumza wakati wa kufunga Kampeni hizo, Dkt. Chakou Tindwa mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani, amesema kuwa Katika Mabadiliko ya maeneo bora yaliyofikiwa vizuri ikiwemo maji na umeme ambavyo jitihada hizo zimefanywa na diwani pamoja na mbunge.
“Tanzania tupo juu, kuliko majirani zetu kutokana na viongozi bora tulio nao tuache porojo za kwenye mitandao na kila mtu ahakikishe anakwenda kutiki.

“Hivyo naomba nichukue fursa hii,kumuombea kura za kishindo kwa mgombea urais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia makamo wake Dkt.emmanuel Nchimbi,Mbunge wetu Dkt Seleman Jafo na pia mgombea udiwani Aidan Kitale.

“Mkoa wa Pwani tumekuwa tano Bora mambo muhimu ni kushinda na kukipatia chama kura nyingi, hivyo basi kila mwananchi ahakikishe siku ya tarehe 29 asitoke peke yake atike na jirani yake waende kutiki na kuchagua viongozi wa CCM kwa sababu Wana uwezo wa kutosha kupeleka gurudumu mbele, amesema Dkt Tindwa.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako