Na Agnes Alcardo, Timesmajira Onlne. Dar
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema Serikali chini ya chama hicho itahakikisha Kivuko cha Mv-Magogoni na Mv-Kigamboni, vinakarabatiwa kwa haraka ili kuwapunguzia adha wakazi wa maeneo ya Kigamboni.
Dkt. Nchimbi amesema hayo Septemba 28, 2025 akihutubia wananchi wa Kigamboni kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Mji Mwema, Kigamboni,jijini Dar-es-Salaam.

Dkt. Nchimbi amesema,miongoni mwa changamoto zinazowakabili wakazi wa maeneo ya Kigamboni miongoni ni pamoja na ukosefu wa vivuko hivyo, ambapo ametoa ahadi ya kushughulikiwa kwa wakati.
Sanjari na hayo, amesema endapo CCM itapata tena ridhaa ya kuongoza nchi, katika miaka mitano ijayo, itaendelea kupeleka miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu ya barabara na nyingine katika Jimbo la Kigamboni.Hivyo ameomba wananchi hao wakipigie kura chama hicho.
Ambapo watajenga shule za msingi nne kati ya hizo tatu kati zitakuwa za mchepuo wa kiingereza kuanzia darasa la kwanza,pia shule za sekondari tano ambazo zitakazojengwa kwa mtindo wa ghorofa pamoja na ujenzi wa chuo cha Veta cha Kigamboni.
Pia amesema, Serikali itaboresha hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ili itoe huduma za kibingwa zaidi, ujenzi wa vituo vipya vya afya sita, ikiwemo kukamilisha kituo cha Afya cha Mji Mwema ambacho kinaendelea na ukarabati.
Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, ikiwemo ya Kibada hadi Mwasonga, Mji Mwema hadi Pemba Mnazi, Kibugumo hadi Serikali za Mitaa pamoja na barabara za mitaa kujengwa kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Fullshangwe, Geza Ulole, Geza Juu, Muongozo, Kibugumo Darajani na ujenzi wa Makaravati katika maeneo ya Cheka, Kichangani na Ngamia.
Kadhalika Dkt.Nchimbi,amesema Serikali hiyo itaboresha makazi ya Kigamboni kwa kutoa hati za viwanjakwa wakazi wa maeneo hayo huku akisisitiza kuendelezwa kwa maeneo yaliyoachwa ili kupunguza mapori na kuleta maendeleo.

Hata hivyo akihutubia wananchi wa Jimbo la Mbagala, Dkt. Nchimbi amesema, Serikali itahakikisha inajenga stendi ya mabasi ya kisasa, itakayokuwa na maduka, ujenzi wa bandari kavu ya Kurasini, itakayoongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo na ajira.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi