Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Shinyanga
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,amewaahidi wananchi wa Isaka kuwa endapo chama hicho kitapata ridhaa kwa mara nyingine kuongoza nchi,mwakani watakamilisha ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), kipande kilichobaki cha kilomita 37.
Dkt.Nchimbi,amesema hayo Septemba 4,2025,wakati akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama, jimbo la Msalala, kwenye mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika mkoani Shinyanga.

Pia ita jenga vituo viwili vya afya ambapo kimoja kitajengwa eneo la Segese na Manase, madarasa 112, maabara 20 na mabweni 21 katika shule za sekondari.
Aidha itaongeza skimu za umwagiliaji kutoka 15 hadi 20,masoko matatu, maghala 90, sehemu za kuogeshea mifugo maarufu majosho 10 na upatikanaji wa umeme kila kijiji.
“CCM imedhamiria kufanya mambo mengi ya maendeleo katika Mji huu wa Isaka.Haya yote yatafanyika endapo wananchi mtaendelea kuiamini CCM na kukipa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi yetu,”amesema Dkt. Nchimbi.
Sanjari na hayo Dkt.Nchimbi,alimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala Mabula Magangila pamoja na Madiwani wa CCM.

Hata hivyo Dkt.Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako