Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Kilimanjaro
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema,serikali chini CCM, imekusudia kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami na changarawe wilayani Mwanga.
Miongoni mwa barabara ambazo zitaboreshwa ni pamoja na kumalizia kipande cha kilomita 13 cha barabara ya Cleopa Msuya.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo Septemba 14, 2025, kwenye mkutano na wananchi, uliofanyika kwenye uwanja wa Cleopa Msuya,ikiwa ni muendelezo wa kukinadi chama hicho ili wananchi wakipigie kura katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
Dkt. Nchimbi amesema,mbali na uboreshwaji wa miundombinu pia kitahakikisha inajenga stendi ya mabasi itakayokuwa na maduka na kukamilisha mradi wa maji ambao tayari umeanza, ili ufikie asilimia 95.
Amesema, huduma za kijamii kama hospitali zitaboreshwa kwa kusogezwa karibu zaidi na wananchi wilayani humo ili waepuke hadha ya kutembea umbali mrefu.

Pia amesema, mashamba darasa ya uvuvi yanaenda kuanzishwa, pamoja kongani za viwanda katika kila wilaya ili kuendelea kutatua changamoto za ajira kwa vijana pamoja na kuongeza vipato katika halmashauri husika.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako