January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga kufunga kampeni zake za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kishindo hapo kesho Novemba 26, 2024 kama kilivyozindua.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2024 Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo CCM Taifa, CPA. Amos Makalla amesema, katika kunogesha mchakato mzima wa kampeni kwa siku saba, yeye ataenda kufunga kampeni hizo mkoani Morogoro hukU Katibu Mkuu wa CCM, Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi akifunga jijini Dar es Salaam.

“Kwa upande wetu CCM kampeni zetu zilienda vizuri na zilikuwa za kistaarabu huku tukiendelea kujizolea maelfu ya wanachama kutoka vyama pinzani kuhamia kwetu hiyo inaonesha wazi kuwa chama chetu kinaenda kuchukua ushindi mchana kweupe,” amesema CPA.Makalla.

Aidha, amewaomba wananchi kuchagua wagombea wanaotokana na CCM na si kuwachanganya na wagombea kutoka vyama pinzani, akidai kuwa kufanya hivyo kutasababisha kurudi nyuma kimaendeleo.

“Mfano umemchagua Mbunge wa CCM au Diwani wa CCM,halafu Mwenyekiti wa Mtaa au Kitongoji kutoka CHADEMA na ukizingatia katika kuleta maendeleo ya sehemu husika wa kwanza ni Mwenyekiti,ambaye ndiye hutoa maeneo kwa ajili ya kufanya maendeleo kama kujenga shule,”.