March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM kufufua viwanda vilivyokufa Njombe

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Njombe

MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,endapo chama hicho kitashinda kitafufua viwanda vyote vilivyokufa mkoani Njombe.

Dkt.Nchimbi amesema hayo,Septemba 24,2025 wakati akisalimiana na wananchi wa Jimbo la Lupembe na kufanya mkutano mdogo kwenye uwanja wa mpira wa Ilunda jimboni humo mkoani Njombe.

Amesema, endapo CCM itapata tena ridhaa ya kushika dola, moja kati ya mkakati wake ni kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi wa Njombe, katika kuanzisha kongani za viwanda kwa kila wilaya.

Pia amesema,miradi ya maendeleo watakayo nufaika nayo wakazi wa Jimbo hilo ni ujenzi wa vituo vya afya vinne, zahanati saba,shule za msingi nne, sekondari tatu na mabweni 20.

Sanjari na barabara zote zitaboreshwa kwa kiwango cha lami na changarawe, hali itayoleta unafuu kwa wakazi hao.