Na Queen Lema,Timesmajiraonline,Moshi
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)Jimbo la Moshi Mjini limezindua rasmi kampeni zake huku mgombea Wa ubunge Ibrahimu Shayo akitoa ahadi za kufanya Jimbo hilo kuwa miongoni mwa Majimbo Bora Tanzania.
Akiongea na Maelfu ya wananchi Septemba 8,2025 Mgombea huyo,amesema kuwa wananchi wanatakiwa kumpa ridhaa ili aweze kutekeleza ahadi zake.
Akitaja ahadi hizo,Ibrahimu amesema kuwa Moshi,wanakabiliwa na changamoto kubwa ya takataka ambapo pia kuna uhaba hata wa magari ya kubebea taka hizo na mpaka sasa hiyo ni moja ya Agenda yake kubwa.
“Moshi takataka ni shida magari ya uchafu yamechoka sana na hata bado hayapiti kwa wakati nataka niwahakikishie kuwa ninapoingia hilo halitakuwepo usafi utakuwa kila mahali”amesema
Hata hivyo amesema kuwa ahadi nyingine ambayo ataitekeleza ni pamoja na ukarabati wa miundombinu ya barabara ambapo ni nguzo mojawapo ya kuchochea maendeleo.
Alidai kwa sasa miundombinu mingi imeharibika vibaya na siyo rafiki lakini atakapofika bungeni atahakikisha kuwa anarekebisha suala hilo.
Aliendelea kudai kuwa katika sekta ya maendeleo akipata ridhaa ya kuwa mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha viwanda vinazaliwa kwa wingi ili viweze kuchochea maendeleo.
“Moshi ni moja ya maeneo ambayo yamebarikiwa kuwa na matunda mengi lakini hakuna kiwanda cha kuchakata matunda hayo sasa nawahaidi kuwa nitahakikisha kuwa tutafufua na kuzalisha viwanda vipya.
Naye kada maarufu wa CCM ,Namelok Sokoine aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha kuwa wanatoa kura za kishindo kwa wagombea wote kuanzia ngazi za udiwani,ubunge na Rais.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako