Na Mwandishi wetu,TimesMajira Online
CHAMA cha Mapinduzi ( CCM) tawi la Amana Dar es salaam limefanya ziara ya kutembelea hospitali ya rufaa ya amana kwa lengo la kuona utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanyika kituoni hapo.
Ziara hiyo imeenda sambamba na utoaji wa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni za kufulia, katoni za maji katika wodi ya akinamama wajawazito nakuahidi kufanya maboresho katika. maeneo yote korofi yanayoizunuka hospitali hiyo.
Akizungumza Dar es salaam Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) tawi la amana Balozi Kindamba amesema wanahitaji huduma bora za afya na rafiki kwa watanzania.
”Tumeona amana inayobadilika ambapo ni tofauti na siku zilizopita hivi sasa kituo chetu kinaonekana kufanya vizuri na kupandishwa hadhi ya kuwa rufaa, “amesema Kindamba
Aidha amesema wao Kama chama kupitia Ilani yao ya CCM watatekeleza yale yote yatakayo Kuwa ni changamoto ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma safi na salama.
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali hiyo Bryceson Kiwelu amedai huduma wanazozitoa zinazingatia kanuni na sheria zinazowataka wataalamu wa afya kuwa nazo katika kuihudumia jamii.
Amesema hivi sasa hospitali hiyo kutokana na kuimarika kwake inatoa Huduma za aina 2 kibingwa na za kawaida ambapo kwa mwaka wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi wa rufaa.
Wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dokta Samia kwa kuwapatia fursa wezeshi za mafunzo kwa wauguzi hao sambamba na uongezaji wa vifaa tiba ikiwemo mashine za CT Scan na uboreshaji wa vyumba vya maabara.
Nae Diwani wa viti maalumu wa CCM kata ya Ilala ambaye pia mlezi wa kituo hicho Mama Zainabu Hoti amewashukuru wauguzi hao na kuwasihi wawe na ushirikiano na wawazi pindi wanapokuwa na changamoto.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango