Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Kilimanjaro
MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema CCM haiwezi kubadili utaratibu wake wa kujali maisha ya wananchi.
Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Septemba 13, 2025 kwenye uwanja wa Snow View, uliopo eneo la Bomang’ombe, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wakati akisalimiana na wananchi wa eneo hilo, alipokuwa akielekea kwenye mkutano katika Jimbo la Siha, ikiwa ni muendelezo wa kampeni za CCM, akikinadi chama na kumuombea kura za ndiyo Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.

Amesema, kuelekea katika miaka mitano ijayo, Serikali chini ya CCM endapo itapata tena ridhaa ya kushika dola, itaendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wa eneo hilo, ikiwemo kuondokana na tatizo la uhaba wa maji, uboreshwaji wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami na changarawe kwa maeneo yote yenye barabara mbovu.
Nyingine ni kuanzishwa kwa kongani za viwanda katika kila wilaya kwa kuzingatia uzalishaji mkubwa wa eneo husika na ufikishaji wa umeme kwenye kila Kaya.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako