March 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Dar yahamasisha wananchi kujiandikisha daftari la mpiga kura

Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Dar

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar-es-Salaam,Jacob Siay,amewataka wanachama wa chama hicho na wananchi wa Jiji hilo,kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata uhalali wa kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Siay amesema hayo wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Magomeni Wilaya ya Kinondoni,ambapo zoezi hilo la kuboresha daftari la mpiga kura katika Mkoa huo limeanza Machi 17 na linatarajiwa kukamilika Machi 23, 2025.

Amesema ili wanachama na wananchi waweze kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi waowataka wakati wa uchaguzi mkuu, wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Pia amefafanua kuwa kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Mkoa huo una jumla ya watu zaidi ya milioni 5.3,83,728, ambao ndio Mkoa wenye makadirio ya wapiga kura wengi kuliko Mikoa yote hapa nchini.

“Hivyo CCM Mkoa wa Dar-es-Salaam tumefanya hamasa ya kutosha katika Wilaya zetu zote ili kuhakikisha viongozi, wanachama na wananchi wanajitokeza kwa wingi katika kuboresha taarifa zao na kujiandikisha kwa vijana waliofikisha umri wa kupiga kura mwaka huu,”.