*Mgombea Urais asisitiza milo minne kwa kila mwananchi
*Kugawa viwanja kwa kila mwananchi
*Mikopo kutolea bure
Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Kijamii,(CCK),David Mwaijojele,ameahidi maisha bora kwa kila mtanzania ikiwemo milo minne kwa siku endapo atapata ridhaa katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
Pia ameahidi kila mtanzania kupatiwa nyumba na kiwanja pamoja na kuwapandishia mishahara askari wa jeshi la polisi.
Mwaijojele amezungumza hayo Septemba 25,2025 na wananchi wa Kata ya Pasiansi jimboni Ilemela mkoani Mwanza,ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kunadi sera ya chama hicho na kuomba ridhaaya kuweza kupigiwa kura ,mkutano uliofanyika uwanja Pasiansi stendi.
“Nikiwa Rais nitahakikisha Watanzania hawajuti kuishi katika nchi yao kwani wengi wanatamani kuishi Marekani.Haipaswi watanzania kulala njaa na kutangatanga kwenye nchi yao kama wakimbizi .Nikiwa Rais nitahakikisha mnakula milo mitatu hadi minne,”amesema Mwaijojele.
Amesema wananchi wanapata tabu ya kuingia kwenye mikopo ya kausha damu kwa sababu ya ugumu wa maisha wakati huo unakuta mtu mmoja kajirundikia mabilioni ya fedha hivyo lazima aeleze fedha hizo kazipata wapi.
“CCK tumejipanga kila mmoja awe na kiwanja chake,tutakuwa na benki Tanzania ya Maendeleo kwa ajili ya kuwatoa Watanzania kwenye umaskini na kuwapunguzia makali ya maisha,ambayo wataenda kuchukua mikopo bure na kuondokana na mikopo ya kausha damu hivyo kila mtu awe na mpango wa biashara,”.
Amesema,atagawa pikipiki na bajaji mpya kwa vijana,kuhakikisha vijana wote wanaoa na wataweka sheria ya kusimamia jambo hilo pamoja na kuanzisha kamati ya maadili ya kushughulika suala la wadada wanaovaa nguo fupi.
Pia amesema,endapo chama chake kitashika dola na yeye kupata ridhaa ya kuwa Rais,atahakikisha kila mtu anakuwa na shughuli za kufanya na kuacha kukaa vijiweni ambako wamekuwa wakitamani kwenda Marekani na South Africa.
“Kila mtu atakuwa na kitu cha kufanya na atajikita kutafuta wateja na kujiingizia kipato huku polisi kazi yao itakuwa kuhakikisha hakuna kijana mzururaji na anayewaza kwenda Marekani, kwani hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile,”.
Sanjari na hayo amesema ilani ya uchaguzi ya CCK ya 2025-2030, ina vipaumbele vingi ikiwemo ajira,maji na vitu vingine vingingi kwa ustawi wa taifa.
“Namewaomba wana Mwanza kunichagua mimi,Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCK,ili tukafanye mageuzi katika Serikali.Baada ya kushinda na kuwa Rais nitachukua ilani za vyama vingine na kuchanganya pamoja ili kupata kitu bora zaidi kwa ustawi wa taifa na kuwa na serikali ya kila mmoja kuchangia kwa kipaji chake,”.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCK,Masoud Abdallah,amesema ili wananchi waondokana na shida zinazowakabili basi wasifanye makosa ifikapo Oktoba 29,2025 wakipigie chama hicho kura za ushindi kwani ndio chama pekee kinachoweza kuleta mabadiliko.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi