March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Canada,UNFPA waimarisha huduma ya Afya ya mama na mtoto Tanzania 

Na Bakari Lulela,Timesmajira

IMEELEZWA kuwa hatua muhimu ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga nchini Tanzania,UNFPA kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na serikali ya Canada kupitia Global Affairs Canada imekabidhi rasmi vifaa vya kazi, mavazi ya kujikinga kwa wahudumu wa Afya ya jamii pamoja na magari mawili.
Ambapo ufadhili wa Dola million 11.75 za Canada zimeonyesha mafanikio 

Akizungumza  wakati wa kukabidhi vifaa kwenye hospitali ya mnazi mmoja jijini Dar es salaam mgeni rasmi katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amesema zoezi hilo ni hatua muhimu ya serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassani kuhakikisha wanawake wanapatiwa huduma stahiki vipindi vya ujauzito na malezi bora kwa watoto wao.

“Sina budi kuongeza jitihada za TAMA na AMREF zilizo chini ya miradi wa thamini uzazi salama ambapo miradi huu unawawezesha akina mama kupatiwa tiba maalumu wakati wa ujauzito na vipindi vya malazi kwa watoto wao kwa kuhakikisha unapata chanjo dhidi ya maladhi mbalimbali,”  

“Hii siyo tu vifaa au magari: ni kuhusu kuimarisha msingi wa mfumo wetu wa Afya tukiwajengea  uwezo wahudumu wetu na kuwapa kipaumbele katika upatikanaji wa huduma bora za matibabu nchini ambapo hakuna mwanamke atakayepoteza maisha wakati wa kujifungua amesema Mpogolo 

Aidha Mpogolo amesema kuwa miradi huu umewezeshwa kwa kutoka serikali ya Canada kutokana na jitihada za serikali ya Tanzania kupitia kwake Dkt Samia Suluhu Hassani imejipambanua kwa kutaka akina mama na watoto wachanga wanapatiwa huduma bora za afya na Kuna kwamba mama ndio kitovu cha afya hivyo ni wajibu apatiwe huduma bora stahiki kwa wakati.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini Mark Bryan amesema wahudumu wa Afya ya jamii ni kiungo muhimu katika familia na mfumo wa huduma za vifaa vya afya ambapo vifaa vilivyokabidhiwa vitawezesha kutoa taarifa sahihi, kufanya marejeo kwa wakati na kutoa huduma inayookoa maisha kwa watoto hususani katika maeneo ya pembezoni na yaliyo na upatikanaji mdogo wa huduma za afya.

Nae Balozi wa Canada nchini Tanzania Emily Burns amesema Canada inajivunia kwa kushirikiana na Tanzania katika juhudi hizi, kuwekeza kwa wakunga na wahudumu wa Afya ni kuweza katika utu, usawa wa kijinsia na mustakabali Bora wa familia za kitanzania.
 
Ameeleza magari yaliyokabidhiwa yataongeza ufanisi wa usimamizi, kuratibu na huduma za uhamasishaji kuhakikisha kila jamii inafanikiwa pia mradi huu umechangia malengo ya maendeleo endelevu (SDG 3) na dira ya maendeleo ya Tanzania 2050 kwa kuimarisha mfumo wa Afya kuanzia ngazi ya jamii.