Na Zena Mohamed,Dodoma
MTHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Charles Kichere amesema
madeni ya michango ya wanachama ambayo hayajalipwa katika mfuko wa bima ya afya shilingi ni bilioni 11.56
Kupitia Ripoti ya kuu ya mwaka ya ukaguzi ywa serikali kui kwa mwaka 2022/23 amesema Kifungu cha 9 cha Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kinawataka waajiri waliosajiliwa kuwasilisha michango inayodaiwa kwa mwezi husika ndani ya siku 30 baada ya mwisho wa mwezi.
“Jumla ya michango iliyokuwa inadaiwa hadi kufika tarehe 30 Juni 2023 ilikuwa shilingi bilioni 42.57, kati ya hiyo, michango ambayo zinadaiwa Taasisi za Serikali ni shilingi bilioni 19.04 sawa na asilimia 45 na shilingi bilioni 23.53 sawa na asilimia 55 zinajumuisha madeni kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali,”amesema.
Amesema katika uchambuzi zaidi alibaini kuwa, kati ya michango yote ya wanachama inayodaiwa na Mfuko wa Bima ya Afya, michango ya shilingi bilioni 19.6 (sawa na asilimia 40) inadaiwa zaidi ya siku 30.
Aidha, mfuko ulikusanya shilingi bilioni 5.34 ya madeni hadi kufikia mwishoni mwa Novemba 2023 na kuacha deni linalodaiwa la shilingi bilioni 11.56.
Ametaja sababu kuu zinazochangia madeni ya muda mrefu ya michango inayodaiwa kutoka mashirika ya umma, ni urasimu katika kuthibitisha madeni.
Amesema hali hiyo inasababisha kuwa na mkusanyiko wa madeni ya muda mrefu kutoka mashirika ya umma, jambo ambalo linaathiri hali ya kifedha ya Mfuko wa Bima ya Afya.
“Madeni ya muda mrefu yanasababisha changamoto za ukwasi kwenye mfuko, hivyo huweza kuathiri shughuli za mfuko, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwalipa watoahuduma kwa wakati.
Hivyo amependekeza; (a) Serikali ihakiki malimbikizo ya michango iliyobaki na kuidhinisha kwa ajili ya malipo; na (b) Mfuko wa Bima ya Afya uendelee kufuatilia madeni ambayo bado hayajalipwa na kuhakikisha kiasi chote kinakusanywa.
17.8
“Hali ya uhimilivu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa ukipata hasara kwa miaka mitano iliyopita. Mfuko umepata hasara ya shilingi bilioni 156.77 kwa mwaka wa fedha 2022/23, ikiwa ni uimarikaji kutoka hasara iliyopatikana mwaka wa fedha 2021/22 ya shilingi bilioni 205.95,”amesema Kichere.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba