January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CAF yakanusha uvumi huu

Na Mwandishi Wetu Timsmajra Online

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu barani Afrika (Caf), limekanusha uvumi huu, kuhusuKombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwezi ujao linaweza kuondolewa kutoka Cameroon kufuatia ugunduzi wa hivi karibuni juu ya aina mpya ya Omicron ya Covid-19.

Aina hiyo mpya ya virusi vya corona imesababisha vikwazo vya usafiri kuanzishwa na baadhi ya nchi kwa mataifa kadhaa ya Afrika, huku Nigeria, ambayo jirani na Cameroon, ndiyo ya hivi punde zaidi kuongezwa kwenye ‘orodha nyekundu’ ya Uingereza.

Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya mashirika ya vyombo vya habari yamependekeza tarehe za mchuano huo wa timu 24 zinaweza kubadilika au hata eneo kuhamishwa,na kupelekwa Qatar.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mawasiliano wa Caf Alex Siewe amesema, sio shirikisho wala maafisa wakuu wa Cameroon ambao wamejadili matukio kama hayo.

“Hatuwezi kuendelea kutumia muda kushughulika na uvumi,” aliambia BBC Sport Africa.

“Hatukupokea ujumbe au taarifa nyingine yoyote kutoka kwa viongozi wetu, hakuna kitu kama hicho cha kubadilisha tarehe au nchi. Hatukujadili mambo kama hayo wakati wa mikutano yetu yote iliyopita.
Tuko kwenye tovuti. Tunafanya kazi.”

Michuano ya barani Afrika, ambayo tayari yamecheleweshwa kwa sababu ya janga la corona, yanatarajiwa kuanza Januari 9 huko Yaounde na kumalizika mnamo 6 Februari.

Wafanyakazi wa Caf waliwasili Cameroon wiki hii kuandaa fainali za Afcon. “Ujumbe rasmi kutoka Caf umetolewa na katibu mkuu Veron Mosengo-Omba anajiunga nasi baada ya siku mbili,” aliongeza.

Chama cha Vilabu vya Ulaya, chombo huru kinachowakilisha vilabu Ulaya, kimeelezea “wasiwasi wake mkubwa” kuhusu ustawi wa wachezaji kabla ya mashindano, na kuongeza kuwa hali ya afya ya umma “inaendelea kuzorota kwa njia ya kutisha”.