March 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BUWSSA yapokea bil.28.1 ya miradi,serikali awamu ya sita

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda(BUWSSA)imesema tangu serikali ya awamu ya sita kuanza Mamlaka hiyo  imepitishiwa miradi ya thamani ya bil. 28,180,572,033.71 na tayari bil. 11,894,976,776.81 zimepokelewa
na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo Machi 6,2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA Esther Gilyoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na muelekeo wa Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Gilyoma amesema upotevu wa maji kwa mwaka 2021 ulikuwa watani wa asilimia 64 kutokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972, baada ya jitihada kubwa za Serikali ya awamu
ya sita za kutoa fedha za kubadili bomba chakavu na mita goigoi upotevu wa maji kwa sasa ni asilimia 32 na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika.

Ameeleza kuwa mwaka 2021,Mamlaka ilikuwa inatoa huduma ya maji kwa wastani wa masaa 12 kutokana na ufinyu wa mtandao na kutokuwa na maji ya kutosha,kwa mwaka 2023 baada ya mradi mkubwa
wa kusafisha na kutibu maji Nyabehu Bunda kukamilika.

“Kwa sasa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda inatoa huduma ya majisafi kwa wastani wa masaa 22 bila ya kuwa na mgawo wa maji, baada ya miradi miwili kukamilika ambayo kwa sasa inaendelea mradi wa kusambaza maji Wariku na mradi wa maji Kisangwa,Mamlaka itatoa huduma ya maji kwa masaa 24 na kufikisha wastani wa utoaji wa huduma kwa wastani wa asilimia 96 na kufikia lengo la Ilani ya
chama cha mapinduzi (CCM).

Akizungumzia Mipango na Mikakati ya Mamlaka hiyo amesema kuwa kujenga mfumo wa mtandao wa maji taka na mfumo wa majitaka wa bomba ili kuzidi kuweka mazingira ya Mji wa Bunda salama.

Pia Ujenzi wa tangi kubwa la maji kwenye mwinuko (elevation) ya 1537m mlima Nyiendo lenye uwezo wa kubeba lita 5,000,000 Kuongeza uwezo wa kuhifadhali maji hasa pale umeme unapokatika na
kusababisha huduma kusimama na kupunguza vituo vya kusukuma maji ili kupunguza gharama za umeme.

“Vilevile tuna Ujenzi wa tangi kubwa la maji lenye uwezo wa kubeba lita 670,000 kwenye kituo cha kusukuma maji Migungani
Ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji kituo cha kusukuma maji Migungani.

“Ujenzi wa tangi kubwa lenye uwezo wa kubeba lita 225,000 kwenye kituo cha kusukuma maji Mugaja ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji kituo cha kusukuma maji Mugaja,Ujenzi wa tangi la maji lenye uwezo wa kubeba lita 150 Kisangwa ili Wananchi wa Kisangwa waweze pata maji kwa njia ya mseleleko.

Lakini pia Ujenzi wa upanuzi mtandao wa bomba 300mm toka Migungani hadi Mlima bomani kuongeza uwezo wa kusukuma maji mengi mjini Bunda kwa kutumia pampu mbili na Ujenzi wa mtando wa bomba toka kituo cha kusukuma maji Migungani hadi mlima Nyiendo Kuongeza wingi wa maji
mjini Bunda.