May 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bussungu,Khatibu kupeperusha bendera ya ADA-TADEA uchaguzi Mkuu

Na Bakari Lulela,Timesmajira

‎‎‎CHAMA Cha African Democratic Party(ADA-TADEA) kimemteua Georges G.Bussungu kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara na Juma Ally Khatibu kuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu nchini kote.‎‎

Akizungumza mara baada ya kupitishwa na Mkutano Mkuu Maalum wa kuchagua wagombea  uliofanyika Mei 10,2025 Kigogo Mbuyuni Jijini Dar es Salaam amewashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kuwapa heshima na dhamana  kubwa katika kupeperusha bendera ya chama pamoja na kuwaamini.‎‎

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Georges Bussungu ametaja miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuwa atahakikisha analeta mapinduzi ya kiuchumi kwa watanzania pamoja na kufanya mabadiliko maeneo tofauti tofauti.‎‎Kwa upande wake Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar ,Juma Ally Khatibu ameahidi kwamba kutokana na kupewa dhamana ya kupeperusha bendera ya chama chake sehemu ya kiinua mgongo chake atakachokipata  baada   Baraza la Wawakilishi kuvunjwa atapeleka pesa kwenye chama ili chama kiweze kufanya kampeni.‎‎

“Bila chama hiki Mimi nisingekuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, bila chama hiki mimi nisingekuwa Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyopita,sehemu ya kiinua mgongo tujue kwamba si changu tutakaa na viongozi wenzangu ili kupanga ratiba ya kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kusaidia watakaogombea kiti cha ubunge na udiwani”, amesema

Khatibu‎Aidha,amesema kuwa watashirikiana  ili chama hicho kiweze kupata kura zakutosha ,kwani Chama Cha ADA-TADEA kinafuata matakwa ya kisheria.‎‎‎

Awali Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza ambaye alihudhuria kushuhudia namna Uchaguzi huo wa ADA-TADEA ukifanyika kwa amani‎amesema Nimeshuhudia kuwa uchaguzi unafanyika vizuri kwa kuzingatia Sheria za nchi na katiba ya Chama chao.‎‎