NA Mwandishi wetu, timesmajira
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa msaada wa bidhaa mbalimbali za chakula pamoja na mahitaji mengine katika kituo cha watoto yatima kinachojulikana kwa jina la AL-Zam Orphanage Center kilichopo Mbagala Zakhiem Wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na mafuta ya kupikia, ,sukari, unga wa sembe, mchele, maharage, nyama, sabuni, madaftari, dawa ya meno, miswaki, pipi, na kalamu.
.
Afisa Leseni kutoka BRELA Koyan Abubakar akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu ,Godfrey Nyaisa ameeleza kuwa lengo kubwa ni kuwatia moyo watoto na uongozi wa kituo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya ili kuongeza juhudi ya kuwahudumia wahitaji ili kufikia ndoto zao.
.
“BRELA ni Taasisi inayosimamia Sajili za kibiashara na Leseni, imefika katika kituo hiki kwakuwa ni sehemu ya jukumu la Taasisi la kurejesha kwa jamii mbali na majumu ya msingi ya Taasisi”, amesema Koyan.
Kwa upande wake Afisa Msajili Mwandamizi, Lugano Mwampeta amewaeleza watoto wanaolelewa katika kituo hicho baada ya kueleza ndoto zao katika moja ya nyimbo walizoimba kuwa, njia kuu ya kuzifikia ndoto zao ni kwa kufuata mafundisho wanayopatiwa na walezi wao kituoni hapo.
“Njia kuu ya kufikia ndoto zenu ni kufuata mafundisho mnayopatiwa na walezi hapa kituoni, pia ili muweze kufikia ndoto hizo ni kufanya bidii katika masomo shuleni”, amefafanua Mwampeta.
Mkurugenzi wa kituo hicho Zainab Said Buleta, ameishukuru BRELA kwa msaada huo ambao utawawezesha watoto hao kujikimu.
Zainab ameongeza kuwa, kituo hicho kilianza kwa kuwalea watoto 10 lakini hivi sasa kinalea watoto 60 kati ya hao 35 ni wasichana na 25 ni wavulana.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi