Na Iddy Lugendo, Timesmajira online
BRELA yaja na wiki ya suluhisha “WIKI YA SULUHISHA NA BRELA” kwa ajili ya kusikiliza malalamiko, changamoto mbalimbali kutoka kwa wanahisa, wakurugenzi wa makampuni ambazo wamekuwa wakikutana nazo na kuwakutanisha kwaajili ya kujadili kwa pamoja ili makampuni yaweze kuendeshwa vizuri na kufanya biashara katika mazingira mazuri.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13, 2022 jijini Dar er salaam kaimu mkurugenzi wa idara ya makupuni na majina ya biashara (BRELA) Meinrad Rweyemamu amesema lengo la wiki ya suluhisha na Brela kumekuwa na wamiliki wa makampuni kutaifishwa pamoja na kuwepo kwa migogoro katika makampuni yao, hiyo kupitia wiki hii wataweza kupata suluhisho la migogoro inayowakumba.
“Kwenye Kampuni mwenye hisa hutokea amefariki huku ndugu hawafahamu kinachoendelea kwenye kampuni, hawafahamu zile hisa za marehemu ni mali kama mali zingine ambazo zinagawiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Njoo katika wiki hii tutakuwa pamoja, tutaangalia haki yako ni ipi”. Amesema Rweyemamu
Aidha amesema watakaa na wamiliki pamoja na wahusika kujadiliana na kupeana elimu mwisho wa siku kila mtu apate haki yake na kuondokana na migogoro ambayo imekuwa ikitokea kwenye makampuni mbalimbali.
Hivyo wiki ya suluhisha na Brela inayoanza leo Juni 13, 2022 na kufikia tamati siku ya jumapili Juni 19,2022 wenye makampuni wametakiwa kufika eneo husika ambalo ni Makumbusho ya Taifa Posta Jijini Dar es Salaam ili waweze kutatuliwa changamoto zao.
More Stories
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini
Rais Mwinyi: Barabara Pemba zitajengwa kwa lami