Na David John, TimesMajira Online, Geita
WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amewaagiza Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), kuhakikisha wanapambana na watu wanaotumia jumbe fupi kwa njia ya mitandao kwa lengo la kupotosha umma wakijifanya wao ni BRELA wakati si kweli.
Biteko ameyasema hayo leo mkoani Geita wakati akitembelea mabanda kwenye maonesho ya sekta ya madini, yanayoendelea mkoani hapa na kupata fursa ya kufika kwenye banda la BRELA na kusema, lazima taasisi hiyo ya serikali ipambane na watu hao.
“Kuna watu bandia ambao wanasumbua wananachi na wengine kuwaibia kwa kujifanya wao ni wafanyakazi wa BRELA, wakati ni wezi hivyo ni vyema nyinyi mkaweka utaratibu mzuri wa kupambna na kundi hili ambalo linatumia jumbe fupi za kwenye mitandao na kuwarubuni watu kama wao wanafanya usajili,” amesema Biteko.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Makampuni kutoka BRELA, Mainrad Rweyemamu amesema, wao kama taasisi wamepokea maagizo ya Waziri Biteko na watayafanyia kazi lakini hata hivyo, wameshaanza kuchukua hatua kwa baadhi ya watu.
Amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwenye banda la BRELA kwa ajili ya kufanya usajili mbalimbali, ili kujihakikishia na kile ambacho anakimiliki na kuwataka waandishi kuendelea kuwahabarisha wananchi.
%%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais