Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Afya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya sita (6) wa Corona (COVID – 19) na kufikia idadi ya wagonjwa 18 kutoka 12 ambao taarifa yao ilitolewa Aprili 13, 2020.
Miongoni mwa wagonjwa hao Watanzania watano na raia wa Misri mmoja ambaye aliingia nchini Machi 15, 2020 akitokea Misri kupitia Dubai kwa Shirika landege la Fly Dubai.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Visiwani Zanzibar, Hamad Rashid inasema kuwa, wagonjwa wote ambao ni raia wa Tanzania hawana historia ya kusafiri nje ya nchi siku za hivi karibuni.
Amesema, wagonjwa wote wamelazwa katika vituo maalum kwa ajili ya kuendelea na matibabu huku Serikali kupitia Wizara ya Afya ikiendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo zinazotolewa mara kwa mara ikiwemo unawaji wa mikono kwa maji ya kutiririka na sabuni, kuepuka misongamano na kuhairisha safari za nje na ndani ya nchi zisiz.o za lazima.
More Stories
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni
Polisi Mbeya kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Pasaka