Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WIZARA ya Afya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya sita wa Corona (COVID-19) na kufanya idadi ya wagonjwa hao kufikia 24 kutoka 18 ambao tuliowatolea taarifa Aprili 15, mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Zanzir, Hamad Rashid Mohamed ilieleza kwamba wagonjwa hao ni wanaume watatu na wanawake watatu wenye umri kati ya miaka 30, 27, 28, 58, 23 na 55.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wagonjwa wote ni rain wa Tanzania na hawana historia ya kusafiri nje nchi siku za hivi karibuni.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wagonjwa wote wamelazwa katika vituo maalum kwa ajili ya kuendelea na matibabu. Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo zinazotolewa mara kwa mara ikiwemo kunawa mikono kwa maji ya kutiririka na sabuni, kuepuka misongamano na kuahirisha safari za nje na ndani ya nchi zisizo za lazima.
“Wizara inaomba wananchi ambao wana dalili za homa kali, kukohoa na kupiga chafya kujitokeza katika vituo vya afya au kupigasimu namba 190.
Ni vyema mgonjwa mwenye dalili za maradhi hayo asijichanganye na wagonjwa au watu wengine na tuache tabia ya kujitibu wenyewe, kwani kwa kufanya hivyo tutaendelea kueneza maambukizi na vifo vinavyo husiana na ugonjwa huu,” ilieleza taarifa hiyo.
Aidha katika kipindi hiki Serikali imewataka wananchi wanaokwenda kwenye misiba wachukuwe tahadhari na wanawashauri ni vyema washirikiane na wataalamu wa wilaya kwa kupata miongozo stahiki.
Habari kamili katika gazeti la Majira…
More Stories
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi