Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Moscow
Ripoti mpya kutoka Wizara ya Afya nchini Urusi imethibitisha kuwa, maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) yamebainika kuwa chanzo cha kupunguza ubora wa mbegu za kiume na vinasababisha wanaume kuwa tasa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la RT, matokeo hayo yanatokana na utafiti wa kisayansi uliofanywa na wataalam wabobezi katika masuala ya afya nchini humo.
Ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Moscow kupitia mkutano wa kutoa tathimini ya kile ripoti imeainisha juu ya matokeo hayo ya utasa kwa wanaume.
Uvarova amesema kuwa, utafiti umebainisha kuwa, kuna upungufu wa asilimia 38 katika viwango vya ubora wa manii kwa wanaume waliopona virusi vya Corona.
Watafiti wamekuwa wakijadili juu ya athari inayowezekana ya Covid-19 juu ya uzazi wa wanaume tangu janga hilo lilipoanza huko Wuhan nchini China mwezi Desemba, 2019.
Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa, virusi viliathiri mfumo wa uzazi wa kiume na huenda ukaathiri kabisa mfumo huo hivyo kuchangia wanaume wengi kuwa tasa.
More Stories
Watakiwa kushirikiana kutikomeza matatizo ya lishe
CCBRT yazidi kuunga mkono juhudi za Rais Samia
Rais Samia afanya uteuzi