December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Breaking News: Rais Samia amlilia Membe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshtushwa na kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, aliyefariki Dunia muda mfupi uliopita katika Hospitalu ya Kairuki Mkoani Dar es Salaam.

Pia Rais Dtk. Samia ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Membe alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.

Kwa taarifa zaidi endelea kuwa nasi.