Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online Morogoro
WAZIRI wa Mambo Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amepata ajali mkoani Morogoro na amelazwa hospitalini akipatiwa matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare amethibitisha kutokea ajali hiyo leo.
Amesema Profesa Kabudi alipata ajali hiyo njia ya kwenda Dodoma nje kidogo ya Mji wa Morogoro akiwa safari kuelekeza kwenye ziara ya kikazi jimboni kwake Kilosa.
RC Sanare amesema na yeye alikuwa kwenye msafara huo, lakini alikuwa amemtangulia na ndipo walipigiwa simu kwamba Waziri amepata ajali, hivyo ilibidi wakimbie warudi Morogoro na walikuta tayari ameishafikishwa hospitalini.
Amesema alipata bahati ya kumuona anaendelea vizuri, wanamshukuru Mungu madaktari wanaendelea kumhudumia na kwamba hana tatizo kubwa sana.
Ametumia muda huo kuwatoa wasiwasi Watanzania na wananchi wa Kilosa kwamba anaendelea vizuri na baadaye watasikia madaktari wanawashauri.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi