Na Joyce kasiki,Timesmajira online,Dodoma
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha kwa muda mafunzo ya kujitolea ya jeshi hilo kwa mwaka 2020/2021 kwa sababu za ndani ya jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Jeshi hilo Chamwino mkoani Dodoma, Kaimu Mkuu wa Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena amesema kutokana na mafunzo hayo kusitishwa ,vijana wote waliochaguliwa na kuripoti makambini wanapaswa warejee majumbani kwao.

“Kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo,JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa kuripoti kambini kwa ajili kuhudhuria mafunzo ya kujitolea warejee majumbani kwao,” amesema Kanali Mabena.
Kwa wale ambao walikuwa bado hawajaripoti, Kanali Mabena aliwataka wasiende kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa hadi hapo itakapoangazwa tena.
More Stories
Waislamu Mwanza wapokea Ramadhani kwa maandamano ya kidini
Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala,katiba na sheria yaridhishwa ujenzi soko Kariakoo
TRA Tanga yakusanya bil.178.3 kwa miezi sita