January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa

BREAKING NEWS: Housegirl auawa

KISA: Mama mwenye nyumba kuchepuka

Na Jumbe Ismailly, Igunga

MKAZI wa Mtaa wa Stoo Kata ya Igunga Mjini, Ezekieli Jonasi (37) anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Igunga kwa tuhuma za mauaji ya binti wa miaka 16, Esther Mahona mkazi wa Mtaa wa Stoo,Kata ya Igunga mjini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema kwamba tukio hilo limetokea Mei 5,mwaka huu, saa nne usiku katika Mtaa wa Stoo,Kata ya Igunga mjini.

Kamanda Mwakalukwa amefafanua kwamba, mtuhumiwa Ezekeieli Jonasi
alikuwa akiishi na binti huyo kama mfanyakazi wa ndani na ndipo baada ya yeye kutengana na mke wake alimwita ndani binti huyo na kumtaka amweleze ni mwanaume gani aliyekuwa akitembea na mke wake.

Kwa mujibu wa Kamishn Mwakalukwa baada ya binti huyo kuulizwa swali hilo na mtuhumiwa,binti huyo alidai kwamba yeye hajui kitu chochote,jibu ambalo mtuhumiwa hakuridhika nalo.

Habari kamili, soma Gazeti la Majira