Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
KIKOSI cha Uokoaji na Maafa Wilaya ya Ilala, leo kimelazimika kufunga Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam.
Akizungumzia hilo, Afisa Maafa Wilaya ya Ilala Magdalena Msaky amesema, kufuatia kufungwa kwa Barabara hiyo huduma ya mabasi ya mwendo kasi (DART), yatapita barabara ya Kigogo na Mkwajuni ili kufika Kariakoo, Kimara, Morocco na Kivukoni.
“Eneo la Jangwani kwa sasa sio salama kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha jiji la Dar es Salaam na Ukanda wa Pwani, hivyo tumelazimika kufunga barabara hii kuanzia saa 11.45 asubuhi,” amesema Msaky.
Msaky amewashauri wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kupita katika njia mbadala tofauti na eneo la Jangwani ambalo kwa sasa si salama.
%%%%%%%%%%%
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi