Na Esther Macha, Mbeya
HATIMAYE Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wananchi wa Kiwira Wilaya ya Rungwe wamefanikiwa kumtia nguvuni kijana Eliakim James (20) kwa tuhuma za kumuua bibi yake Junes Sankanye(65) na kisha kutokomea na kichwa chake.
Kitendo hicho kilipelekea familia kulazimika kuzika kiwiliwili bila kichwa baada ya kumtafuta mtuhumiwa na kichwa cha marehemu siku mbili bila mafanikio.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkunga Mariam Bachu Nurdin alieleza mkasa mzima wa tukio hilo la mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa na kichwa hicho na kuleta simanzi kubwa katika Kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ulrich Matei alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo ambaye ametafutwa kwa siku mbili tangu afanye mauaji hayo.
Habari kamili ipo katika gazeti la Majira …
More Stories
TAKUKURU yanasa watuhumiwa wa wizi wa mali za wakulima
CCM yampongeza Rais Samia kutunukiwa tuzo na Bunge
Mwenge wazindua Miradi saba Temeke