December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: AICC yapata Mkurugenzi mpya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Christine Gideon Mwakatobe (Pichani kulia) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Mwakatobe alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Uteuzi huu unaanza mara moja.