RIO DE JANEIRO, Brazil
TIMU ya taifa ya Brazil imefanikiwa kutinga fainali ya Copa America baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Peru katika mchezo wa Nusu Fainali usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Nilton Santos Jijini Rio de Janeiro.
Katika mchezo huo, Pongezi pekee zimuendee mfungaji wa bao, kiungo wa Lyon ya Ufaransa, Lucas Paquetá dakika ya 35 akimalizia pasi ya nyota mwenzake wa Ligue 1, Neymar wa PSG.
Kufuatia matokeo hayo,Brazil itacheza na mshindi wa nusu fainali nyingine ya Usiku wa leo kati ya Argentina na Colombia katika mbio za kuwania taji la fainali itakayopigwa Maracana siku ya Jumamosi.
More Stories
Kasulu FC mabingwa mashindano Khimji 2025
Fainali Khimji cup kufanyika Februari 7,2025
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu